Event

ZITUNZENI BOTI HIZI - Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba

  • 2026-08-14 16:48:06

Na:Sweetbetter Njige

Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amezitaka mamlaka zinazohusika na ulinzi baharini kuzitunza boti  za doria  PB SAILFISH 02 na PB SAILFISH 03 alizozipokea na kuzizindua  Ijumaa tarehe 31 Julai 2026 tukio lililofanyika katika Viwanja vya Bandari ya Dar es Salaam. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Nchemba ameziagiza mamlaka husika kutenga bajeti ya uendeshaji wa boti hizo mbili za kisasa ili zitumike kwa muda mrefu kuzuia uvuvi haramu na uharamia baharini na hivyo kutoa mchango stahiki wa kufikiwa kwa malengo ya Dira 2050. Aidha amewashukuru wadau wa maendeleo ambao wameendelea kutoa mchango wa maendeleo ya Taifa. 

“Naishukuru Serikali ya Japan, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na wadau wengine wa maendeleo kwa kufadhili mradi huu na miradi mingine muhimu kama huu, mradi huu umeleta manufaa makubwa zaidi ya ununuzi wa boti za doria ikiwemo kuandaliwa kwa mwongozo wa Kitaifa wa kukabiliana na uhalifu baharini, ujenzi wa miundombinu ya kukaushia samaki, utoaji wa mafunzo kwa wakulima wa mwani na kuwajengea uwezo wataalamu wa Tanzania.

“ Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuimarisha usalama wa mipaka ya maji na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na usalama kwa wananchi”

Akizungumza katika halfa hiyo Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini anayeshughulikia Taalumu Profesa Provident Dimoso kwa niaba ya Mkuu wa Chuo amesema

“Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, tunajisikia fahari kutoa mchango wetu wa maendeleo nchini kupitia wataalamu wetu kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa, UNDP. Tunaahidi kuendelea kufanya kazi kwa  uadilifu, uwazi na weledi mkubwa kwa manufaa ya Taifa letu. 

Chuo cha Mipango kwa kushirikiana na UNDP wamewezesha ununuzi wa boti hizi mbili  zilizopewa majina PB Sailfish 02 na PB Sailfish 03 kwa ufaadhili wa  Serikali ya Japan kupitia mradi wa Enhancing Maritime Surveillance in Tanzania’s Coastal Waters Amidst the Red Sea Crisis.

Boti hizi  zimenunuliwa kwa  dola za Kimarekani Milioni 1.6.

Subcribe weekly newsletter
Register Now