Wahitimu wa Kidato cha Sita na Diploma Kanda ya Kaskazini wamehimizwa kuchangamkia fursa ya kutuma maombi ya kujiunga na chuo katika dirisha la awamu ya tatu kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza kwa kuchagua programu zitolewazo na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini chenye Kampasi mbili za Dodoma na Mwanza.
Rai hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Profesa Provident Dimoso Oktoba 06 na 07, 2024 alipozungumza na Wananchi wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara kupitia vituo vya Radio vya Moshi FM, Garaxy Fm na Sun Rise Fm alipofanya mahojiano ya moja kwa moja kwa nyakati tofauti katika ziara ya kutembelea vituo vya redio vya Kanda ya Kaskazini.
“Shime kwa Vijana mliohitimu Kidato cha Sita na Diploma ambao kwenye dirisha la kwanza na la pili hamkupata fursa kwa sababu mbali mbali mtumie fursa ya dirisha hili la tatu ambayo imetolewa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kwa siku tano kuanzia Oktoba 05 hadi 09, 2024 kutuma maombi ya kujiunga na Chuo cha Mipango kwa njia ya mtandao ya oas.irdp.ac.tz na kuchangua program mbali mbali zitolewazo na Chuo kwani nafasi bado zipo Chuo cha Mipango” Alibainisha Profesa Dimoso.
Pia amewahimiza wananchi wa Kanda ya Kaskazini kuchangamkia fursa ya Shahada za Uzamili “Masters” zitolewazo na Chuo cha Mipango kwani dirisha bado liko wazi hivyo kwa Watumishi waliopo Makazini na Wadau mbali mbali kuchangamkia fursa hiyo ya kujiendeleza kielimu kupitia Chuo cha Mipango.
Sambamba na hili Profesa Dimoso amebainisha kuwa Chuo mbali na kuwaandaa Wanafunzi katika fani za kitaaluma pia Chuo hulea vipaji vya wanafunzi wake katika masuala ya ujasiliamali na ubunifu kupitia Kituo cha Ubunifu na Ujasiliamali ambapo huwawezesha wahitimu kujiajiri wenyewe.
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kilianzishwa mwaka 1979 kwa sheria ya Bunge Namba 8 ya mwaka 1980 kwa madhumuni ya kuboresha shughuli za upangaji mipango ya maendeleo vijijini kwa njia ya kuandaa wataalam wa mipango na kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watendaji na viongozi