Wanawake wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ( IRDP) leo Jumatano tarehe 8 Machi , 2023 wanaungana na Wanawake wengine Duniani katika kusheherekea Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo kwa Mkoa wa Dodoma inafanyika katika Viwanja vya Sabasaba Wilayani Kondoa
Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.
Kauli Mbiu ni " Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia, Chachu katika Kuleta Usawa wa Kijinsia".