Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, alitembelea Banda la Chuo katika Maonesho ya Nanenane 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma.
Prof. Mayaya alishiriki katika siku ya kilele cha Maonesho hayo, yaliyoambatana na hafla ya kufungwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Chuo alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na timu ya Maonesho pamoja na kutoa pongezi kwa timu kwa ushiriki na kuendelea kuutangaza mchango wa Chuo katika mipango ya maendeleo vijijini.
Register Now