MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

Serikali kuongeza Bajeti Uboreshaji wa Miundombinu ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.

  • 2024-11-24 22:52:04

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb) amesema Serikali itaendelea kukiwezesha kibajeti Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) ili kiweze kuwa na miundombinu na rasilimali watu inayokidhi mahitaji ya utoaji wa elimu kwa viwango bora.

Akizungumza kwa niaba ya Mhe. Dkt. Nchemba katika Mahafali ya 38 duru ya kwanza yaliyofanyika katika Kampasi Kuu ya Dodoma, Kamishina wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja alisema ili kuboresha sekta ya elimu nchini Serikali inakusudia kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Dkt. Mwamwaja alisema kuwa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa muda mrefu kimekuwa kikipitia kwenye mafanikio makubwa kutokana na mikakati iliyojiwekea hasa ile ya kuwainua wananchi kiuchumi kupitia program mbalimbali ikiwemo uanzishwaji wa Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (Mipango Enterprenurship and Innovation Centre - (MEI)), pamoja na miradi inayoendeshwa na wabia wa maendeleo wakiwemo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United Nations Development Programme – UNDP).

Alitumia Mahafali hayo kuushauri Uongozi wa Chuo kupanua wigo wa miradi katika upande wa miradi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili huduma hiyo iwafikie wananchi wengi zaidi na waweze kunufaika na fursa zinazotokana na huduma hizo.

‘’Aidha, kwa upande wa miradi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ninawashauri kupanua wigo wa maeneo mengine ya nchi ili wananachi wengi zaidi wanufaike na huduma zenu na kwa kufanya hivyo mtawasaidia kujikwamua kiuchumi’’ aliongeza Dkt. Mwamwaja.

Dkt. Mwamwaja kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe.Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) aliwataka wahitimu na wananchi kwa ujumla kujitokeza na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba,2024, Uchaguzi ambao ni muhimu katika kuimarisha demokrasia na ushiriki wa wananchi katika utawala wa nchi yao.

Subcribe weekly newsletter