MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

Tuzo ya Usimamizi Bora wa Rasilimaliwatu na Utawala Bora

  • 2024-12-22 16:54:46

Mkuu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa. Hozen Mayaya akipokea Tuzo ya Mshindi wa pili wa Usimamizi Bora wa Rasilimaliwatu na Utawala kwa Taasisi za Elimu ya Juu hapa nchini kutoka kwa Afisa Rasilimaliwatu na Utawala Mwandamizi Bwana Joseph Chiwanga. Tukio hilo lilifanyika wakati wa hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Viongozi wa Menejimenti Chuo Cha Mipango yaliyofanyika Hotel ya St. Gaspar jijijini Dodoma siku ya Ijumaa tarehe 20 Desemba, 2024.

Tuzo hiyo ilitolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Mkutano wa Wakuu wa Idara za utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma uliofanyika Jijini Dodoma tarehe 17 - 19 Desemba 2024.

Subcribe weekly newsletter