MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

WAKULIMA WA MAZAO BAHARI WATAKIWA KUWA MFANO BORA

  • 2024-10-18 14:33:12

Wakulima wa mazao ya bahari ya mwani na jongoo bahari Wilayani Bagamoyo wametakiwa kuwa mfano kwa wakulima wengine baada ya mafunzo elekezi watakayopata ya uendeshaji wa kilimo kisasa; usimamizi wa vikundi; usimamizi wa fedha; kuongeza thamani ya mazao pamoja na masoko katika Mradi wa Bahari Maisha.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bwana Shauri Selenda katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa vikundi vya wakulima wa mazao bahari iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Septemba 23, 2024.

Bwana Selenda alisema vikundi vyote ambavyo vimepata fursa ya mafunzo hayo kuhakikisha wanayazingatia mafunzo hayo ambayo yatawafanya kuwa vikundi vya mfano kwa wanabagamoyo na Taifa kwa ujumla.

“Nawaomba baada ya mafunzo haya muende mkawe mfano kwa vikundi vingine hivyo mtumie fursa hii ya mafunzo kwa kujifunza kweli ili mtoke na kitu kitakacho wasaidia kwa kuendesha kilimo chenu kisasa zaidi” Alisema Bwana Selenda na kuongeza “fursa hii ya uwepo wa bahari tuliyonayo tukiitumia vizuri tutafanya maendeleo makubwa kupitia kilimo cha mazao bahari”.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Bahari Maisha Dkt. Bonamax Mbasa ambae ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Mipango amesema Mradi huo wa Bahari Maisha unaotekelezwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hadi sasa umenufaisha jumla ya wakulima 294 kupitia mafunzo haya elekezi katika maeneo ya Unguja, Pemba na Tanga.

Subcribe weekly newsletter