Event

KIKAO CHA KAMATI YA FEDHA, MIPANGO NA MAENDELEO YA WAFANYAKAZI CHA BARAZA LA UONGOZI WA CHUO

  • 2026-08-14 17:03:01

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Mipango, Ajira na Maendeleo ya Wafanyakazi ya Baraza la Uongozi wa Chuo, Bw. Benjamin Chilumba (kushoto), akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika tarehe 7 Agosti 2026.

Pamoja na mambo mengine, Kamati ilipokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za Fedha, Mipango, Ajira na Maendeleo ya Wafanyakazi kwa Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha 2025/26 (Aprili hadi Juni 2026), Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2025/26 hadi kufikia Robo ya Nne, na Taarifa ya Masuala ya Mazingira, Jamii na Utawala Bora (ESG).

Mambo mengine ni Kupokea na kujadili  Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kamati ya Uadilifu wa mwaka 2025/26 pamoja na Mpango wa mwaka 2026/27, Taarifa ya Utendaji Kazi za Watumishi (PEPMIS) na Taasisi (PIPMS) kwa mwaka 2025/26, pamoja na Rasimu ya Sera ya Malazi ya Wanafunzi ya mwaka 2026

Subcribe weekly newsletter
Register Now