Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mheshimiwa Rashid Hadid Rashid (kulia), akimkabidhi tuzo Afisa Mikopo wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Bwana Joseph Kilihindi (kushoto), kufuatia Chuo hicho kufanya vizuri katika kusimamia masuala ya mikopo ya wanafunzi.
Tukio hilo limetokea kando ya Kikao Kazi cha ZHESLB kati ya Maafisa Mikopo wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu, kilichoendelea Wete, Pemba, Zanzibar, leo Jumanne tarehe 10 Februari, 2026.
Aidha, tuzo hiyo inatambua uwezo wa Chuo kuandaa na kuwasilisha taarifa za malipo kwa usahihi na kwa wakati. Kati ya Vyuo zaidi ya 110 vya kati na vyuo vikuu nchini, IRDP imekuwa miongoni mwa Vyuo 15 vilivyopokea tuzo hiyo, ikionyesha kuthaminiwa kwa mchango wake katika kusimamia masuala ya mikopo ya wanafunzi.
Register Now