MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

WAHITIMU WA MAFUNZO YA MAZAO BAHARI WATAMBULIWE WILAYANI BAGAMOYO - Mheshimiwa Amiry Mpwimbwi

  • 2024-10-18 14:43:45

Wahitimu wa vikundi vya wakulima wa mazao bahari ya kilimo cha mwani, ufugaji wa jongoo bahari na kaa Wilayani Bagamoyo watambuliwe katika ngazi zote za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kama wakufunzi wa Ufugaji wa mazao bahari .

Rai hiyo imetolewa na Diwani Kata ya Dunda Mheshimiwa Amiry Mpwimbwi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mheshimiwa Mohamed Usinga katika hafla ya ufungaji wa mafunzo elekezi kwa vikundi vya wakulima wa mazao bahari iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Jumamosi Septemba 28, 2024.

"Mafunzo haya juu ya uendeshaji kilimo; Usimamizi ya Vikundi ; Usimamizi wa Fedha; Kuongeza Thamani ya Mazao pamoja na masoko ya mazao bahari yaliyofadhiliwa na Shirikia la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kutelezwa na Chuo cha Mipango ni fursa ya kipekee na ni muhimu kwa wakulima hao ambao wanakwenda kuwa wakufunzi kwa wakulima na wafugaji wengine Wilayani hapo" amesema na kuongeza

“Nawaagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo kupita Maafisa Uvuvi mliopo hapa kuhakikisha Wanufaika hawa wanatambulika kuanzia ngazi ya Kaya hadi Kata na kuhakikisha wanatoa mafunzo haya kwa kuwapangia programu maalumu ambayo italeta mabadiliko chanya katika sekta ya uchumi wa blue”. Alisema Mhe. Mpwimbwi.

Aidha, Mheshimiwa Mpwimbwi amelishukuru Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa ufadhili wa Mashine ya kuchakata zao la Mwani katika Wilaya ya Bagamoyo ambayo inakwenda kuongeza thamani ya zao hilo bahari ambapo ameahidi usimamizi madhubuti wa mashine hiyo itakapoanza kufanya kazi Wilayani hapo.

Kwa upande wake Mratibu Mkuu wa Kitengo cha Jumuiya ya Wadau wa Maendeleo wa Kimataifa wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ambrose Mugisha. amesema Shirika limedhamiiria kuhakikisha linashirikiana na Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi katika Mradi huu wa Bahari Maisha kwa kuwalenga makundi ya Wanawake na Vijana.

Pia ameahidi kuwa kupitia Mraadi huu changamoto nyingi zinakwenda kutatuliwa  na kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao bahari ambapo mbali na mashine ya kuchataka mwani pia shirika kupitia mradi huo linatoa Boti katika maeneo ya Tanga, Unguja, Pemba na Bagamoyo ambazo zitatumika katika kilimo cha mazao bahari. 

Kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo haya wametoa shukrani kwa wafadhili na wakufunzi wa mafunzo haya na kuahidi siyo tu kushirikiana na wakulima wengine wa mazao bahari bali pia kusambaza maarifa hayo kwa wakulima wengine ambao hawakunufaika na mafunzo hayo.

Mwanakikundi  wa Kikundi cha Kiwawaba Bw. John Daniel Assey amesema “kwa kweli tunawashukuru sana wakufunzi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na maafisa uvuvi wetu kwa sasa tunaenda kuboresha ufugaji wetu kisasa zaidi”

Mradi wa Bahari Maisha unaotekelezwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) unalenga  kuboresha kilimo cha mazao ya baharini ya mwani, ufugaji wa jongoo bahari na kaa katika maeneo ya Tanga, Unguja Pemba na Bagamoyo.

Subcribe weekly newsletter