MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

MIPANGO WATOA MSAADA WA MASHUKA ST. GEMMA HOSPITALI.

  • 2024-07-02 09:21:54

Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini leo Jumatano tarehe 19 Juni, 2024 kimetoa msaada wa mashuka 100 kwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Dodoma St. Gemma.

Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yenye kaulimbiu "Kuwezesha kwa utumishi wa umma uliojikita kwa umma wa Africa ya karne ya 21 iliyojumuishi na inayostawi, ni safari ya Mafunzo na mabadiliko ya Kiteknolojia"

Akiongea baada ya kukabidhi Mkuu wa Chuo cha Mipango Profesa Hozen Mayaya amesema "Msaada huu ni kuunga mkono juhudi Sekta binafsi katika kutoa huduma za jamii kwa wananchi. Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa sekta binafsi kuendesha shughuli zao zikiwemo huduma za jamii na Afya. Kwa msingi huo tunaona tunawajibu wa kutoa msaada kwa hospitali hii ambayo ni msaada mkubwa kwa jamii yetu ya Chuo", alisema na kuongeza " tutaendelea kutoa ushirikiano kwa hospitali hii kila tutakapo pata uwezo".

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St. Gemma iliyoko Miyuji, jirani na eneo la Chuo cha Mipango , Dkt. Erick Mbunga aliushukuru uongozi wa Chuo na wafanyakazi wote kwa moyo wa kujitoa.

"Tumeguswa na ukarimu wenu kwetu. Hii si mara ya kwanza. Ninakumbuka hata miaka ya nyuma katika maadhimisho haya mlitupatia misaada ya mashuka na vifaa vingine. Hivyo, kwa dhati ya moyo wangu ninaomba mpokee shukrani zetu za dhati kwa msaada huu wa mashuka. Tunaomba ushirikiano huu udumu kwa manufaa ya taasisi zetu na taifa kwa ujumla".

Chuo cha Mipango pamoja na matendo hayo ya huruma pia wanatumia maadhimisho hayo kukusanya maoni na kero kutoka kwa wadau wa ndani na nje kupitia madawati yaliyowekwa maeneo mbali mbali ya Chuo. Kuna jumla ya madawati matano.
ya kukusanyia maoni hayo na kero kwa Kampasi zote za Dodoma na Mwanza.

Aidha, ratiba inaonesha Mkuu wa Chuo atapata fursa ya kuongea na watumishi wa Chuo msisitizo ukiwa ujazaji wa fomu za tathmini ya Utendaji wa Kazi kwa njia ya mtandao iitwayo PEPMIS.

#Kupanga ni Kuchagua

Subcribe weekly newsletter