Event

MIPANGO NI MSINGI WA MAENDELEO ENDELEVU - DKT. KOMBA

  • 2026-02-19 13:33:28

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA),Dkt. Andrew Komba  amesisitiza umuhimu wa mipango kama msingi wa taaluma na maendeleo endelevu wakati akitoa mhadhara katika “Public Lecture on Planning” iliyoandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Jana  tarehe 19 Februari 2026, katika Ukumbi wa Mihadhara LT4, Jengo la Pili la Taaluma, Kampasi ya Dodoma.

Katika wasilisho juu ya “Planning as the Foundation of Academic and Development Practices”, Dkt. Komba alisema kuwa mipango madhubuti ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za kitaaluma na maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanafikiwa kwa ufanisi na tija. "Bila mipango, taasisi na mataifa hushindwa kufikia malengo yao kwa wakati na kwa ubora unaotarajiwa", alisema Dkt. Komba.

Mhadhara huo uliwakutanisha wanazuoni wa masula ya Mipango wa ndani ya Chuo na nje kwa lengo la kuimarisha uelewa wa dhana ya Mipango kama msingi wa taaluma na maendeleo hasa katika kipindi hiki cha mapinduzi ya sayansi na teknolojia. 

Kwa mujibu wa Mratibu wa mhadhara huo Dkt. Steven Mwaseba, kufanyika kwa mhadhara huu ni sehemu ya jitihada za IRDP katika kuendeleza mijadala ya kitaaluma na kushirikisha wadau mbalimbali katika kujenga fikra pana kuhusu mchango wa mipango katika maendeleo ya Taifa.

Subcribe weekly newsletter
Register Now