MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

MIPANGO WAENDELEA KUGUSA WAHITAJI

  • 2024-07-02 09:25:57

Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kimeendelea kugusa wahitaji kwa kutoa misaada mbalimbali , Safari hii walioguswa ni Kituo cha Kulelea watoto Yatima kwa jina la The Heart House of Hope Orphanage Home cha Kijiji cha Kanyama, Kata ya Bujora Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Wakiwa na nyuso za bashasha watumishi wa Chuo cha Mipango, Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa wakiongozwa na Mkuu wa Chuo Profesa Hozen Mayaya walifika kwenye Kituo hicho cha Kulelea watoto yatima kutoa misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma .

"Tumejiwekea utaratibu wa kutumia Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kurudisha sehemu kwa jamii na mwaka huu tumetoa misaada ya Mashuka kwa Hospitali teule ya Wilaya ya Dodoma St. Gemma kule Dodoma na Kituo hiki cha Kulelea Watoto Yatima kwa Mkoa wa Mwanza" alisema Profesa Mayaya na kuongeza.
"Ujio wetu una lengo la kuwatia moyo kwa kazi kubwa ya kitume mnayoifanya ya kulea watoto yatima."

Afisa Ustawi wa Jamii Bw. David Mbasha Akiongea kwa hisia baada ya kutolewa kwa misaada hiyo amesema " tunawashukuru sana wenzetu wa Chuo cha Mipango kwa misaada hii. Ninaomba kutumia fursa hii kuwaomba wadau wengine kushiriki na kituo kuwapa watoto wetu furaha na matumaini kupitia matendo haya kihuruma".

Katika tukio hilo la leo Ijumaa tarehe 21 Juni , 2026, Chuo cha Mipango kimekabidhi kwa Kituo hicho cha Watoto Yatima magodoro 20, Kilo 100 za sukari, na kilo 100 za mchele. Misaada mingine ni mafuta ya kupikia lita 40, miche 25 ya sabuni, madaftari 100 pamoja na madaftari makubwa 50.

Kituo cha The Heart House of Hope Orphanage Home kilianzishwa mwaka 1989 kwa lengo la kulea watoto yatima. Kwa sasa kina jumla ya watoto 29 kati yao wakiume 14 na wakike 15 wakihudumiwa na wafanyakazi 7.

#Kupanga ni Kuchagua

Subcribe weekly newsletter