MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

-

  • 2024-06-04 00:36:15

MATUMIZI YA TEHAMA KICHOCHEO CHA MAENDELEO - PROFESA DIMOSO

Na Mariam Mayunga, Dodoma

Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Provident Dimoso amesema matumizi ya TEHAMA ndiyo msingi wa maendeleo katika dunia ya sasa. Profesa Dimoso ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 3, 2024 wakati akifungua Warsha Juu ya ufundishaji kwa kutumia TEHAMA. Warsha hiyo ya siku nane inawashirikisha wahadhiri wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini inalenga kuwajengea uwezo katika ufundishaji kwa kutumia TEHAMA ilikwenda na kasi ya kukua kwa sayansi na teknolojia.

''Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa TEHAMA kwa maendeleo ya nchi imeamua kutumia elimu ya juu kuleta mageuzi ya kiuchumi ambapo msisitizo uko kwenye matumizi ya TEHAMA. Hivyo, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ikiwa ni moja ya taasisi nufaika na Mradi huu wa Mageuzi ya Kiuchumi kupitia Elimu ya Juu ( Higher Education for Economic Transformation- HEET) hapa nchini hatuna budi kuandaa mitaala inayohimiza matumizi ya TEHAMA", alisema Profesa Dimoso.

Alimkaribisha Profesa Dimoso kufungua mafunzo haya, Mratibu wa Mradi HEET Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Bwana Said Abdallah Panga amewataka washiriki kuwa makini ilikuijua kwa kina mifumo mbalimbali watayakayofundishwa kwa minajiri ya kuleta mageuzi ya kitaaluma kwa Chuo chao..

Wawezeshaji katika warsha hiyo inayojumuisha washiriki 67 ni Bwana Fadhili Ngalawa, Charles Mulisa na Stephen Lugaimukamu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini pamoja na Dkt. Everist Mtitu kutoka Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia ambaye ni mratibu wa HEET Kitaifa.

Kwa mujibu wa Mratibu wa HEET , Chuo cha Mipango Bwana Panga, jumla ya washiriki 67 watapata mafunzo hayo kwa awamu mbili kuanzia leo Jumatatu Juni 3, 2024 hadi Juni 15, 2024 yatakapofungwa na Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya.

#Kupanga ni Kuchagua

Subcribe weekly newsletter