MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

HALMASHAURI ZAFUNDWA MBINU ZA UJUMUISHI WA MASUALA YA UHIMILIVU NA MABADILIKO YA TABIANCHI KWENYE MIPANGO NA BAJETIĀ 

  • 2025-09-04 13:58:41

HALMASHAURI ZAFUNDWA MBINU ZA UJUMUISHI WA MASUALA YA UHIMILIVU NA MABADILIKO YA TABIANCHI KWENYE MIPANGO NA BAJETI 

Na Andrew Mallya,  Morogoro

Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI kinatekeleza Mradi wa Mabadiliko ya Tabianchi unaofadhiliwa na Mfuko wa Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF - LoCAL).  Katika  kutekeleza mradi huu, Chuo cha Mipango kinaendesha mafunzo kwa wataalamu wa serikali za Mitaa kutoka Halmashauri nane  zinazonufaika na mradi huu.

Akiongea siku ya kwanza ya mafunzo haya yanayofanyika Ukumbi wa EDEMA , Manispaa ya Morogoro    mratibu wa mafunzo haya Profesa Omari Mzirai amezitaja halmashauri hizo  kuwa ni pamoja na Mpwapwa, Kondoa, Chamwino, Mkinga, Mafia, Mtwara, Mtama na Kigamboni.

Kwa mujibu wa Profesa  Mzirai lengo la mafunzo haya ya siku nne ni  kuwajengea uwezo wataalamu wa Serikali za Mitaa katika kujumuisha masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na uhimilivu katika Mipango na bajeti za Halmshauri zao. 

Washiriki wa mafunzo haya ni wataalamu kutoka idara mbalimbali za Halmashauri ikiwemo Mipango, Fedha, Kilimo, Uvuvi, Mifugo na waratibu wa Mradi wa LoCAL kutoka katika Halmashauri shiriki. 

Wawezeshaji wa mafunzo haya ni  Profesa Omari Mzirai, Profesa Innocent Zilihona,  Dkt. Christina Geofrey pamoja na Dkt. Aron Bakari. Wengine ni Bwana James Maghori, Bwana Sostenes Nakamo, Bi Fausta Senga na Bi Neema Nnko

Subcribe weekly newsletter
Apply Now