Wakulima wa Mwani Kisiwani Pemba watakiwa kuendelea kuunga mkono juhudi za wadau wa maendelo kwa kuweka jitihada katika uzalishaji wa zao hilo katika ubora wa hali ya juu kwa kutumia vafaa vya kisasa walivyopewa na Chuo cha Mipango kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia Mradi wa Bahari Maisha.
Wito huo umetolewa na Afisa Mdhamini, Wizara ya Uchumi wa Buluu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ofisi ya Pemba Dkt. Salim Mohamed Hamza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kuzalisha na kuchakata zao la mwani kwa vikundi vya wakulima wa zao hilo iliyofanyika katika Soko la Mboga Mboga na Samaki - Tumbe, Mkoa wa Kaskazini Pemba Jumapili Desemba 15, 2024.
“Tumekuwa ni vikundi vya wakulima wa zao la mwani ambao tumepata bahati kubwa sana ya kupata mafunzo ya namna bora ya kulima zao hili na jinsi ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara zetu kutoka kwa wadau wetu wa maendeleo UNDP kupitia Chuo cha Mipango". Alisema Dkt. Hamza na kuongeza, " leo tunakabidhiwa vifaa hivi vya kisasa hivyo niwaombe mkazingatie yale mafunzo mliyoyapata mkazalisha mwani katika ubora wa hali ya juu kuunga mkono juhudi za wadau wetu wanao wanatamani kuona maisha yetu ya mkulima mmoja mmoja wa zao hili yanakuwa bora”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa – Mwanza Prof. Juvenal Nkonoki ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanziabar (SMZ) kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonesha katika hatua zote za utekelezaji wa Mradi wa Bahari Maisha unaotekelezwa na Chuo cha Mipango kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Nae Afisa Kilimo cha Mwani – Pemba Bibi. Aisha Khamis Sultan amewahakikishia wadau wa maendeleo ambao ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuwa kwa usimamizi madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kipaumbele ni uchumi wa buluu hivyo akiwa msimamizi wa Kilimo cha mwani katika eneo la Pemba atahakikisha vikundi hivyo vinakwenda kupiga hatua kubwa kwa zao hilo kuwa katika ubora wa Kimataifa.
Awali akitoa ufafanuzi wa makabidhiano ya