MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

Mafunzo ya Muda mfupi huongeza Ufanisi kwenye utekelezaji wa Majukumu yenu

  • 2024-02-19 05:27:32

Mafunzo ya Muda mfupi huongeza Ufanisi kwenye utekelezaji wa Majukumu yenu

Na Mariam Mayunga

Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA) wanaoshiriki mafunzo ya muda mfupi ya Usimamizi wa Miradi, Ufuatiliaji na Tathimini wametakiwa kuongeza Ufanisi kwenye utekelezaji wa majukumu yao baada ya kupata mafunzo haya.

Rai hiyo imetolewa leo Jumamosi 17 Februari 2024 na Mkurugenzi wa Utafiti na Ushauri Elekezi Dkt. Hosea Mpogole wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini katika hafla ya kufunga mafunzo ya muda mfupi ya Usimamizi wa Miradi, Ufuatiliaji na Tathimini (Project, Designing, Implementation, Monitoring and Evaluation).

" Kupitia mafunzo haya mkatekeleze ufatiliaji na tathimini ya miradi iliyopo katika maeneo yenu kwa lengo la kuleta tija kwa taasisi yenu ya TAWA na Taifa kwa Ujumla".

Mafunzo hayo ya siku sita yaliyoanza Jumatatu tarehe 12 Februari 2024 Jijini Dodoma yamehitimishwa leo Jumamosi tarehe 17 Februari 2024, yakiwa na washiriki 29 kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA).

Mratibu wa Mafunzo ya muda mfupi wa Chuo Cha Mipango Bwana Benjamini Magori ameahidi kuendelea kuratibu mafunzo yenye kujibu changamoto za utekelezaji wa majukumu sehemu za kazi.

Wawezeshaji wa Mafunzo hayo ni Bw. Charles Mulisa na Bw. Tito Mwamanyeta wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.

#Kupanga ni Kuchagua

Subcribe weekly newsletter