Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya akifurahia Tuzo ya Mshindi wa Kwanza wa Usimamizi Bora wa Rasilimaliwatu na Utawala kwa taasisi za Elimu ya Juu hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ofisini kwake na Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Bibi Sarah Mgabo ( wa kwanza kushoto). Wengine katika picha ni Makamu Mkuu wa Chuo - Mipango, Fedha na Utawala Profesa Canute Hyandye ( wa pili kulia) na Afisa Rasilimaliwatu na Utawala Bwana Joseph Chiwanga ( wa kwanza kulia).
Tuzo hiyo ilitolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Mkutano wa Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma uliofanyika Jijini Arusha tarehe 11 Oktoba 2023 hadi tarehe 13 Oktoba 2023
Mwaka jana Chuo cha Mipango kilishika nafasi ya tatu.