The second round for the Application Window for 2023/2024 is now open apply now
Read MoreMhitimu wa Stashahada ya Maendeleo ya Jamii katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Thabita Pando, akionesha bidhaa anazozalisha.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wamefanikiwa kujiajiri kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazowaingizia kipato.
Mafanikio hayo yamepatikana baada ya wanafunzi hao kupata mafunzo kupitia Kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali cha Chuo cha Mipango maarufu MEI (Mipango Enterpreneurship and Inovation Centre).
Akizungumza na mwandishi wa makala hii Agosti 8, 2023 kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma Utafiti na Ushauri Elekezi), Profesa Provident Dimoso, amesema MEI ni Kituo Atamizi kwa ajili ya kulea mawazo ya biashara ya wanafunzi na kuwawezesha kufikia ndoto zao.
“Kwa kutambua changamoto ya uhaba wa ajira nchini na duniani kote, Chuo chetu pamoja na kuweka moduli za masuala ya ujasiriamali kwa kila programu, pia tumejiongeza kwa kuanzisha Ktuo cha Ubunifu na Ujasiriamali.
“Vijana wote wanaojiunga na Chuo cha Mipango tunawashauri na kuwahamasisha kujiunga na kituo hicho ili wapate fursa ya kujengewa uwezo kwenye masuala mbalimbali ya ubunifu iwe michezo, sanaa au ujasiriamali ambapo kwa wajasiriamali wanaanzisha biashara mbalimbali, wanajiajiri na kuajiri wenzao,” amesema Profesa Dimoso.
Amesema kupitia program hiyo wanafunzi kadhaa wamefanikiwa kubuni biashara akiwemo aliyeshinda tuzo ya mbunifu bora Tanzania na kudhaminiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kupatiwa Sh milioni 40 kuendeleza ubunifu wake.
Kijana huyo ambaye kwa sasa amehitimu aliibuka mshindi katika Mashindano ya Maadhimisho ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) mwaka 2021 katika Maonesho yaliyofanyika Viwanja vya Jamhuri, Jijini Dodoma.
MAKISATU huratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kila mwaka yakishirikisha wabunifu kutoka shule za msingi, sekondari, VETA, vyuo vya ufundi, vyuo vya kati, na vyuo vya elimu ya Juu nchini.
Katika hatua nyingine Wizara ya Fedha kwa kuguswa na shughuli za MEI, imeunga mkono juhudi za Chuo za kuwajengea uwezo wanafunzi wajasiriamali kwa kumuongezea mtaji wa Shilingi Milioni Moja mwanafunzi Thabita Pando ili kuendeleza biashara yake.
Akiongea baada ya kupokea msaada huo Thabitha ameishukuru Wizara ya Fedha kwa msaada huo na kuahidi kuongea ubunifu katika biashara yake.
"Nimejawa na furaha kubwa sana. Msaada huu kwangu ni kichocheo cha kunifanya niongeze bidii ya ubunifu na kutafuta masoko ya bidhaa zangu za pilipili na jam," amesema na kuongeza
"Jam ninayotengeneza ina vitamin C ya kutosha, inasaidia kuimarisha mifupa na utunzaji wa ngozi ya mtu,” amesema Thabita ambaye amefaulu vizuri masomo yake ya Stashahada ya Maendeleo ya Jamii na anategemea kujiunga na Shahada ya Kwanza ya Maendeo ya Jamii mwaka huu.
Mwanafunzi huyo amefanikiwa kusajili jina la biashara yake kwa jina la 'Bitha Afrika’ na kutoa wito kwa wahitimu wa kidato cha nne, kidato cha Sita, Astashahada, au Stashahada wenye maono na ndoto za kijasiriamali na ubunifu kujiunga na Chuo hicho wapate fursa za kuendelezwa.
Amesema malengo yake ya baadaye ni kuwa mfanyabiashara mkubwa na kumiliki kampuni.
Kupitia program hiyo wanafunzi huanza kutambuliwa pindi wanapoanza masomo yao na mpaka sasa MEI inalea wanafunzi zaidi ya 40.
Chuo hicho pia huwaombea mitaji ili kuendeleza bunifu zao huku wakiendelea kusoma.
Serikali imewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kuchangamkia fursa ya upendeleo inayotolewa na sheria ya manunuzi inayozitaka taasisi zote za Serikali kutenga asilimia 30 ya bajeti zao za manunuzi ya mwaka kwa ajili ya makundi maalum katika jamii wakiwemo vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.
Rai hiyo imetolewa jijini Mwanza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo ambaye alimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika mahafali ya 36 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini duru ya pili katika Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, jijini Mwanza.
Bi. Omolo alieleza kuwa kuwa zaidi ya asilimia 70 ya Bajeti kuu ya Serikali hutumika kwenye manunuzi mbalimbali ya bidhaa, huduma na kandarasi za ujenzi na hivyo ni vema wakachangamkia fursa hiyo. ‘‘Bajeti ya manunuzi kwa mwaka huu wa fedha ni takribani Sh. trilioni 32, ambapo asilimia 30 ya kiasi hiki ni takribani sh. trilioni 9.78 ambazo zinapaswa kutengewa makundi haya maalum. Hivyo, niwaase vijana wetu kujiunga katika makundi na kuyasajili rasmi ili yatambulike kuweza kunufaika na fursa hiyo’’, alisema Bi. Omolo.
Alifafanua kuwa Serikali iko tayari kusaidia vijana wenye mawazo chanya ya kibiashara kutimiza malengo yao jambo la msingi ni kujiunga kwenye vikundi vyenye lengo la aina moja ili iwe rahisi kukabiliana na changamoto ya mtaji mdogo kwa kushirikiana na wenzako katika kikundi kuliko mtu akiwa peke yake.
Bi. Omolo aliwaasa wahitimu kuwa na moyo wa uthubutu na kuyafanyia upembuzi yakinifu mawazo yao ya biashara, kuyaandalia mpango wa biashara na kuyatekeleza kwa ufanisi bila kukata tamaa kwani ulimwengu wa leo unahitaji moyo wa kupenda kuendelea kujifunza na zaidi kuwa wabunifu.
Alitoa rai kwa wazazi na walezi kuiunga mkono Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa wahitimu hao kwa kuwawezesha watakaokuwa na mawazo ya kibiashara kupata mitaji ya kuanzisha miradi yao ya biashara. ‘‘Serikali kwa upande wake itaendelea na agenda yake ya kuboresha mazingira ya upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya vijana kupitia mikopo inayotolewa na mamlaka za serikali za mitaa’’ alisema Bi. Omolo.
Pia Bi. Omolo alizitaka Bodi za taasisi zote za umma kuzisimamia vizuri taasisi zinazotekeleza miradi ya ujenzi ili thamani ya fedha ionekane kwani palipo na usimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi Serikali haitasita kutoa fedha za maendeleo.
Aidha, alitoa rai kwa taasisi nyingine za elimu ya juu na kati na ikiwezekana shule za sekondari kuiga mfano wa chuo hicho wa kuwaandaa wataalamu kuwa mahiri na weledi kwa kutumia mfumo unaohusisha nadharia na vitendo, vilevile kozi zenye moduli ya masuala ya ujasiriamali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho, Prof. Martha Qorro, ameishukuru Serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za maendeleo kuwezesha chuo hicho kutekeleza kwa ufanisi mradi wa upanuzi wa chuo.
Pia alisisitiza kuwa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho litaendelea kufanya kazi kwa bidii kwa kukisimamia chuo hicho kuboresha mazingira yake na miundombinu huku likitanguliza maslahi mapana ya Taifa ili kukiwezesha chuo kupata mafanikio zaidi.
Naye Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo ya Vijijini Prof. Hozen Mayaya, alisema kuwa wahitimu hao wamefundishwa na wamefuzu kuweza kuingia katika kutumikia Taifa wakiwa na maarifa na ujuzi stahiki katika soko la ajira ndani na nje ya nchi. Alisema kuwa chuo hicho kimejidhatiti katika kuwaandaa wataalamu wenye weledi wa kutosha katika fani za mipango ya maendeleo, bali pia kutoa huduma iliyo bora kwa wakati na inayokidhi matakwa ya wadau.
Pia aliishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuendelea kukiwezesha Chuo kupata miundombinu ya msingi ambayo ni bora na ya kisasa ikiwemo majengo yaliyowekewa mawe ya msingi na uzinduzi.
Jumla ya wahitimu 2691 wakiwemo wanawake 1491 na wanaume 1200 wamehitimu mafunzo yao na kutunukiwa Astashahada Stashahada na Shahada ya kwanza kwa wahitimu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini katika programu 3 kwenye mahafali ya 36 ya Chuo duru ya pili katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa Mwanza
Read MoreWajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini na baadhi ya Viongozi wa Chuo, Leo Alhamisi Desemba 15, 2022 wamehitimisha mafunzo ya uongozi yaliyoratibiwa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute). Mafunzo haya yamefanyika kwa vipindi tofauti kuanzia Mei 26, 2022.
Read MoreWahitimu wanaohitimu Vyuo mbalimbali nchini wametakiwa kujiunga katika vikundi ili kuchangamkia fursa za fedha za mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu zinazotengwa na serikali kupitia halmashauri zote hapa nchini. Wito huo umetolewa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Fedha na Mipango Bwana . Moses Dulle wakati wa ufunguzi wa kusanyiko la Kitaaluma katika Chuo cha Mipango ambalo pamoja na mambo mengine hutumika kutoa Tuzo kwa wahadhiri na wanafunzi waliofanya vizuri katika kazi na masomo mbalimbali kwa mwaka wa 2021/22.
Bwana Dulle amesema Serikali ya Awamu ya sita imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya ajira yanayowawezesha vijana kujiajiri wenyewe kwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri zote kwa ajili ya kukopesha makundi maalumu wakiwemo vijana.
" Uamuzi huu wa Serikali ni fursa kwa wahitimu wetu ambao wengi wao ni vijana na wanachotakiwa kufanya ni kujiunga katika vikundi vyao na kuvisajili katika Halmashauri walizopo Ili waweze kupata mikopo ambayo inaweza kuwasaidia kutekeleza Miradi ambayo wamejiajiri" . alisema Bw. Dulle.
Aidha Mkurugenzi huyo aliupongeza Uongozi wa Chuo cha Mipango kwa kutekeleza Miradi mbalimbali ya kuendeleza miundombinu ya Chuo na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa msaada utakaohitajika kukusainia Chuo kuboresha mazingira ya kusomea na kufanya kazi. Pia, amewataka wahitimu wa Chuo cha Mipango kuungana na Uongozi wa Chuo katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo kama ambavyo imekua ikifanywa na wahitimu wa vyuo vingine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango Prof. Martha Qorro aliwapongeza wahadhiri na wanafunzi wote waliofanya vizuri na kuwataka kuendelea kutumia ujuzi walionao kwaajili ya kustawisha maisha yao ya Jamii .
Awali Makamu Mkuu wa Chuo - Taluma Prof. Provident Dimoso akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Chuo alisema katika mwaka wa 2021/22 Chuo hicho kimepata mafanikio mengi ikiwemo ongezeko la wanafunzi waliodahiliwa , watumishi pamoja na kutekeleza Miradi ya Ujenzi wa hosteli na vyumba vya mihadhara.
Read MoreMkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Prof. Hozen Mayaya alisema Chuo kimeweka kipaumbele katika kuwajengea uwezo watumishi wake katika maeneo mbalimbali ya ubobezi wao ili wapate stadi stahiki katika kuhudumia umma wa watanzania. "Tunaendelea kuwajengea uwezo watumishi wetu katika mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa lengo la kuwa na rasilimali watu mahiri katika kutekeleza majukumu ya ndani ya Chuo na nje" alisema Prof. Mayaya.
Prof Mayaya ameyasema haya jana Alhamisi tarehe 29 Septemba,2022 alipokutana na timu ya wataaalamu wa Chuo wa Masuala ya Uwezeshaji ofisini kwake waliokwenda kuwasilisha mkakati wa kutoa huduma bora kwa jamii.
Akiwasilisha mkakati huo Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma Prof. Provident Dimoso alisema kwa muda mrefu Chuo kimekuwa na ndoto ya kuwa na kituo cha kuwajengea uwezo wananchi kiuchumi. Ndoto hii ilitimia mwaka 2019 kwa kuanzisha Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu ( Mipango Entrepreneurship and Innovation ) maarufu MEI . Kwa mujibu wa Prof . Dimoso Kituo hiki tangu kuanzishwa kwake kimefanya vizuri katika kulea vipaji vya ubunifu na ujasiriamali kwa wanafunzi wa Chuo cha Mipango. " Mkakati wetu ni kupanua wigo kwa kuwa na programu zinazogusa maisha ya jamii kubwa. Vilevile kuendelea na programu ya kubadilisha mtizamo kwa vijana wetu kuhusu ajira. Msisitizo ni kujiajiri na kuajiri wengine."alisema Prof. Dimoso na kuongeza, "Ujasiriamali ndio ajenda ya sasa, Vyuo vinazalisha wahitimu wengi kila mwaka wakati nafasi za ajira ni chache sana hivyo msisitizo na msukumo uwe mkubwa kwenye masuala ya Ujasiriamali na Ubunifu".
Read MoreMwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijjni Prof. Martha Qorro, Leo Agosti 19, 2022 ameongoza kikao cha 126 Cha Baraza la Uongozi wa Chuo kilichofanyika katika ukumbi wa Maktaba, Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa Mwanza.
Pamoja na mambo mengine Baraza limepokea na kujadili tathinimi ya utendaji kazi ya watumishi (OPRAS) kwa mwaka 2021/22; Limewathibitisha Wakuu wa vitengo wawili na limeridhia kubadili kada kwa watumishi wawili. Vilevile limepokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu kwa Kampasi za Dodoma na Mwanza; Limejadili Rasimu ya Sera ya Usimamizi wa Miliki; Limepitisha Mpango wa Ununuzi wa Vifaa, Ujenzi na Huduma zisizo za Ushauri; na kupitisha Mpango Kazi wa Kamati zake za Taaluma; Mipango, Fedha, Ajira na Maendeleo ya Wafanyakazi; na Kamati ya Ukaguzi.
Kikao hicho cha Baraza la Uongozi kilitanguliwa na vikao vya kamati za Baraza. Siku ya Jumanne Agosti 16, 2022 kilifanyika kikao kimoja cha Kamati ya Ukaguzi kikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati CPA. Dkt. Samwel Werema. Aidha siku ya Jumatano Agosti 17, 2022 vilifanyika vikao viwili vya Kamati ya Taaluma na Kamati ya Fedha, Mipango, Ajira na Maendeleo ya Wafanyakazi vilivyo ongozwa na Prof. Donald Mpanduji na Wakili Grace Mfinanga mtawalia.
Katika hatua nyingine Wajumbe wa Baraza la Uongozi pamoja na Viongozi wa Juu wa Chuo walipata mafunzo ya uongozi wa rasilimali za umma. Mafunzo haya ya siku moja yalifanyika Alhamisi Agosti 18, 2022 yaliendeshwa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) mwezeshaji akiwa Bw. Paul Bilabaye ambae ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Tanzania (PSPTB).
Akifunga Kikao hicho Mwenyekiti wa Baraza ameipongeza Menejimenti ya Chuo kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa majukumu ya Chuo. Wakati huo huo amewahimiza Wanajumuiya wa Chuo cha Mipango kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23 na kutoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa. “Taarifa zitakazo patikana kwenye Sensa ni nyenzo muhimu kwa Mipango ya Maendeleo ya sasa na ya miaka mingi ijayo”. Alisema Prof. Qorro.
Read MoreDkt. Godrich Mnyone (wa kwanza kushoto) ameungana na viongozi wa mkoa na wananchi wa Dodoma katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika kijiji cha Bahi, Wilaya ya Bahi.Dkt. Mnyone alimwakilisha Mkuu wa Chuo Prof. Hozen Mayaya.
Read MoreNa. Nuru J. Mangalili
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Staki Senyamule amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika halmashauri zote nane za mkoa wa Dodoma na kuweka mawe ya msingi, kuzindua, na kukagua miradi ya maendeleo. Mh. Senyamule amesema hayo Jumanne tarehe 16 Agosti alipokuwa anapokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh. Peter Serukamba.
Leo umeanza kukimbizwa katika wilaya ya Bahi na kesho utakimbizwa katika Wilaya ya Dodoma Jiji, ambapo Mwenge wa Uhuru utatembelea na kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa barabara Kisasa nyumba 300, kuweka jiwe la msingi mradi wa kitalu nyumba kikundi cha vijana kiu ya ufanisi Viwanja vya nane nane , kuzindua mradi wa Hotel ya Southern Empire na mradi wa Kituo cha Afya cha Chang'ombe.
Ujumbe wa Mwenge mwaka 2022 ni "Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo Shiriki Kuhesabiwa Tuyafikie Maendeleo ya Taifa".
Read MoreKwenye Maonesho ya Vyuo vya Elimu Juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU) katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Profesa Provident Dimoso amesema kuwa chuo hicho kina tatua changamoto za ajira kwani kimeanzisha kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali kwa wanafunzi wote wanaosoma katika chuo hicho.
Pia amewakaribisha wahitimu wa kidato cha nne kwa ajili ya kujiunga na masomo ya ngazi ya cheti na waliomaliza kidato cha sita kujiunga ngazi ya Shahada 'degree' pamoja na wale ambao ufaulu wao ni wa alama moja ' Principal Pass' nao wanaweza kujiunga na chuo hicho kwa ngazi ya diploma.
" Imekuwa ni utamaduni kwa Watanzania kudhani kwamba ukimaliza kidato cha sita na ukapata alama moja ya ufaulu wanadhani wamefeli mwanafunzi anaweza kuendelea na masomo kwa kusoma masomo ya diploma ya chuo hiki," amesema Prof. Dimoso.
Prof. Dimoso ameongeza chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kinatambuliwa na TCU na kina usajili wa Baraza la elimu na mafunzo ya ufundi (NACTEVET), hivyo mwanafunzi anaposoma Shahada katika chuo hicho uzito wake ni sawa na kusoma chuo chochote duniani kwa kuwa ni kizuri,kina ubora na kimejikita kwenye masuala ya mipango.
KUPANGA NI KUCHAGUA
Read MoreSerikali ya Marekani kupitia Programu yake ya Academy for Women Entrepreneurs (AWE) kwa kushirikiana na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wajasiliamali ili kukua kiuchumi kwa kuwawezesha kutengeneza Mpango wa biashara zao, jinsi ya kukuza mitaji na kuwaunganisha kimtandao na wafanyabiashara waliofanikiwa.
Akizungumza wakati wa Mahafali ya mafunzo hayo yaliyofanyika Jumatatu tarehe 6, Juni, 2022 Chuoni Mipango. Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabiri Shekimweri aliishukuru Serikali ya Marekani kupitia Ubalozi wao nchini Tanzania kwa kuendesha mafunzo hayo muhimu na kuwashauri wanawake hao kuendelea kuchangamkia fursa zinazojitokeza ili kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dkt. Donald Wright aliwapongeza wahitimu hao kwa kumaliza mafunzo hayo, na kuushukuru Uongozi na Menejimenti ya Chuo cha Mipango kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 4 April, 2022 na kuhitimishwa tarehe 6 Juni, 2022. Pia, alisema kuwa Ubalozi wa Marekani umeongeza kiasi cha Dola za Marekani Laki Moja kwaajili ya kuendeleza Programu ya AWE katika Mikoa mingine minne.
Aidha, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Prof. Hozen Mayaya katika hotuba yake alisema Chuo cha Mipango kupitia Kituo chake cha Ujasiriamali na Ubunifu (MEI) kitaendelea kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kuhakikisha mafunzo hayo yanaendelea kutolewa Jijini Dodoma na sehemu mbalimbali nchini.
"Chuo cha Mipango kinayo fahari kubwa kuwa mwenyeji wa mafunzo haya , ambapo baadhi ya wahadhiri wetu walishiriki kuwezesha Programu hii kwa kuratibu na kubadilishana uzoefu na washiriki, pia mmoja wa wahadhiri wetu ameshiriki mafunzo haya ya AWE. Hivyo, ni matumaini yetu kuwa ujuzi na maarifa aliyoyapata yatawanufaisha wanafunzi na Wafanyakazi wa Chuo."Alisema Prof. Mayaya.
Jumla ya Wanawake Wajasiriamali 31 kutoka Dodoma walishiriki mafunzo na walitunukiwa Vyeti kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.
Read MoreChuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) kimetunukiwa Tuzo ya Utendaji Bora katika usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushika nafasi ya tatu Kitaifa katika eneo la Elimu ya Juu na Vyuo Vikuu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea Tuzo hiyo Chuoni Mipango Jumanne tarehe 31 Mei, 2022 Mgeni Rasmi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango Prof. Donald Mpanduji alipongeza kwa hatua hiyo kubwa na kusema kuwa Tuzo hiyo ikawe dira na mwanga kwa wanamipango wote ili kuonyesha ni wapi Chuo kinakwenda.
" Jambo hili ni jambo kubwa na la kujivunia, tuendelee kuchapa kazi na kuyasimamia yale yote tunayoambiwa na viongozi wetu na tufanye kazi kwa kushirikiana pia tuongeze bidii mwakani tushike namba Moja". Alisisitiza Prof. Mpanduji.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kwaajili ya kupokea Tuzo hiyo na kuzungumza na Wafanyakazi wa Chuo cha Mipango , Mkuu wa Chuo cha Mipango Prof. Hozen Mayaya alisisitiza kuendelea kufanya kazi kwa weledi mkubwa na kuendelea kuheshimu vipaji mbalimbali ambavyo watu wanavyo ili kukiwezesha Chuo kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.
Read MoreWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewaasa wasomi kote nchini kushiriki katika Agenda ya utunzaji Mazingira ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuleta Maendeleo nchini. Hayo ameyasema Jumanne tarehe 31 Mei, 2022 Jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na Jumuiya ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) alipofanya Ziara Chuoni hapo ikiwa ni katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani itakayoadhimishwa kitaifa Jijini Dodoma tarehe 5 Juni, 2022. "Tunaona 29.2% ya pato la Taifa linatokana na kilimo hivyo ukame ukishamiri kilimo hakitafanya vizuri na uchumi wa nchi utakua hatarini kwa hiyo tunakila sababu ya kutunza Mazingira yetu." Alisema Dkt. Jafo.
Katika Ziara hiyo Mhe. Dkt. Jafo alitembelea maeneo mbalimbali ya Chuo, kuona shughuli za uhifadhi na usafi wa Mazingira , kuona mradi wa usimamizi wa taka ngumu , mradi wa kuvuna maji ya mvua na kushiriki upandaji wa miti Chuoni hapo na kukipongeza Chuo cha Mipango kwa kuwa na Klabu ya Mazingira inayo shiriki katika ajenda ya utunzaji wa Mazingira.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango Prof. Donald Mpanduji wakati akizungumza kabla ya Mhe. Dkt. Jafo kuongea na Jumuiya ya Chuo cha Mipango alisema kuwa Chuo kimejikita sana kufanya shughuli za Mazingira na kina wataalamu wa kutosha wa Mazingira. "Tunaomba Serikali iwatumie wataalamu wetu wa Mazingira ipasavyo kila panapokua na fursa kwani Chuo kina wataalamu wakutosha". Alisema Prof. Mpanduji.
Aidha , Mkuu wa Chuo cha Mipango Prof. Hozen Mayaya wakati akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Dkt Jafo alisema Chuo cha Mipango kinaendelea kutumia elimu, utaalamu wa mipango katika kuhamasisha Jamii kushiriki Sensa tarehe 23 Agosti,2022.
" Tunatambua shughuli za Mazingira zitakuwa na manufaa zaidi endapo watanzania wote tutajitokeza kushiriki kikamilifu katika Sensa ya Watu na Makazi mwaka huu 2022". Alisisitiza Prof. Mayaya
Read MoreWajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini na Viongozi wengine wa Chuo leo Alhamisi tarehe 26/5/2022 wamepata mafunzo ya siku moja juu ya Akili hisia katika Uongozi ( Emotional Intelligence in Leadership) .
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Hoteli ya Nashera Jijini Dodoma. Mwezeshaji katika Semina hiyo alikuwa Dkt. Lusajo Kajula kutoka Taasisi ya Uongozi. Aidha Semina hii itaendelea katika Vikao vijavyo vya Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.
Read MoreWenyeviti CPA , Dkt. Samwel Werema ( Kamati ya Ukaguzi), Prof . Donald Gregory Mpanduji( Kamati ya Taaluma) na Bw. Michael John ( Kamati ya Fedha) wakijadili mambo mbalimbali yanayogusa maendeleo ya taaluma , ujenzi wa miundombinu pamoja na maendeleo ya wafanyakazi katika Vikao vya Kamati za Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) vilivyofanyika tarehe 24/5/2022 na tarehe 25/5/2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma.
Vikao hivyo vitahitimishwa na Kikao cha Baraza la Uongozi wa Chuo siku ya Ijumaa tarehe 27/05/2022.
Read More[ View More Announcements ]Available Announcements
![]()
LIST OF SELECTED BACHELOR DEGREE APPLICANTS 2023/2024 - SECOND ROUND
Posted: Wed, 20 September, 2023
Attachment [241,68 KB]
![]()
LIST OF SELECTED BACHELOR DEGREE APPLICANTS WITH MULTIPLE SELECTION 2023/2024
Posted: Fri, 25 August, 2023
Attachment [480,04 KB]
![]()
LIST OF SELECTED BACHELOR DEGREE APPLICANTS WITH SINGLE SELECTION 2023/2024
Posted: Fri, 25 August, 2023
Attachment [296,22 KB]
![]()
FIRST ROUND SELECTION FOR BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE APPLICANTS 2023-2024
Posted: Wed, 09 August, 2023
Attachment [742,42 KB]
![]()
MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA ASTASHAHADA YA MSINGI (BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE) KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024
Posted: Wed, 14 June, 2023
Attachment [1,26 MB]
[ View More Notices ]Availalble Notices
![]()
ADMISSION LETTER FOR BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE NTA-LEVEL 4 - 2023/2024
Posted: Mon, 04 September, 2023
Attachment [138,73 KB]
![]()
MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA ASTASHAHADA YA MSINGI (BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE) KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024
Posted: Wed, 14 June, 2023
Attachment [1,26 MB]
![]()
TERMS OF REFERENCE FOR PROVISION OF CONSULTANCY SERVICES FOR DESIGN, PREPARATION OF BIDDING DOCUMENTS, COST ESTIMATES AND CONSTRUCTION SUPERVISION OF ACADEMIC BLOCK AT DODOMA MAIN CAMPUS, MIYUJI AREA
Posted: Fri, 02 June, 2023
Attachment [495,93 KB]
![]()
REQUEST FOR EXPRESSIONS OF INTEREST (REOI)
Posted: Fri, 02 June, 2023
Attachment [285,33 KB]
![]()
IRDP Newsletter 1st Edition
Posted: Tue, 23 May, 2023
Attachment [14,68 MB]
Our Channel